#VIDEO: Vitendea kazi vya usafiri vimekabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma na kutatua changamoto za wananchi kwa haraka, hatua inayolenga kuhakikisha huduma bora na ya uhakika.
Akizungumza Machi 27, 2026 wakati wa hafla ya kukakabidhi yofanyika katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema hatua hiyo inaendana na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, huku vitendea kazi hivyo vikiongeza ufanisi kwa watumishi na kusaidia kuwahudumia wateja kwa wakati.
Aidha, amewahamasisha wakazi wa Kahama kutumia nishati safi ya umeme kupikia kwa kuwa ni nafuu, salama na rafiki kwa mazingira, akibainisha kuwa Serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 600 kujenga laini mpya ya umeme ili kuboresha huduma.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Benson Mbigili, amesema wamepokea magari manne, bajaji moja na pikipiki nne zitakazosaidia kuwafikia wateja hata maeneo magumu na kuendelea kutoa huduma bora huku wakihamasisha matumizi ya umeme kupikia.
#MzawaUPDATE